Serikali ya wanafunzi ARUSO imepokea kwa masikitiko makubwa na inawatangazia wanajumuiya wa chuo kikuu Ardhi kwamba mwanafunzi BUCHUMA HILARIOUS CHRISTOPHER aliyekua akisoma mwaka wa kwanza shahada ya uzamili wa sayansi ya mipango miji na usimamizi (Msc UPM) katika skuli ya SSPSS mwenye namba ya usajili HD/T.1149/2017 amefariki. BUCHUMA amefariki siku ya jumapili asubuhi tarehe 17/12/2017 katika hospitali ya mkoa wa Morogoro kutokana na kuumwa kichwa. Marehemu atasafirishwa kutoka Morogoro siku ya jumatano tarehe 20/12/2017 kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika Geita mjini tarehe 21/12/2017.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa,Jina lake lihimidiwe, AMINA.. |
0 comments:
Post a Comment