Leo tarehe 05/04/2017 Raisi wa serikali ya wanafunzi chuo kikuu Ardhi Mh. KIWANGO, ERASMUS B. amefanya uzinduzi wa blog mpya ya kisasa pamoja na kukabidhiwa kamera na printa kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano, Teknolojia na Machapisho. Uzinduzi huo umefanyika katika jengo la bunge la wanafunzi wa chuo kikuu Ardhi (R-29).
Katika uzinduzi huo Raisi ameeleza lengo kuu na mpango wa serikali kununua kamera na printa kuwa ni kutoa huduma ya upigaji picha hasa siku ambazo wanafunzi wa mwaka wa kwanza wanapokuwa wanaripoti chuoni. Aidha Raisi amesema kupitia kamera na printa  serikali itaweza kuongeza kipato chake.



3 comments:

 
Top