Habari wana-ARU,
Ofisi ya Rais
inapenda kutoa shukrani za dhati kwa ushirikiano mliouonesha katika
msiba wa rafiki yetu, ndugu yetu na mwanachuo mwenzetu JOHN MARTIN.
Viongozi na baadhi ya wana-ARU tuliweza
kufika kijijini kwao Musoma jana mchana na kumpumzisha mwenzetu tukiwa
na uwakilishi kutoka utawala na wanafunzi wapatao 11 na tumerudi wote
salama na tumewasili chuoni leo saa 12 jioni.
Salamu
za shukrani kutoka kwa ndugu na familia yake, wanawashukuru sana kwa
upendo na ushirikiano mliouonesha kwa familia katika kipindi hiki kigumu
wanachokipitia. Nipende kuwashukuru sana kwa
maombi yenu na ushirikiano mliouonesha wa hali na mali katika hili na
tuzidi kushirikiana zaidi na zaidi katika mambo yote.
Mwisho tuzidi kumwombea mwenzetu apumzike mahali pema peponi.
Endelea kutembelea ARUSO BLOG kupata taarifa mbalimbali ewe Mwana-ARU.
Amen
ReplyDelete