WATUMISHI WA CHUO KIKUU ARDHI NA SERIKALI YA WANAFUNZI ARUSO |
Katika kutekeleza agizo la Serikali la kuwataka Wananchi wake, kufanya mazoezi kila juma mosi ya pili ya mwezi uongozi wa Chuo Kikuu Ardhi kwa kushirikiana na idara ya Michezo umewezesha zoezi hilo kwa kufanya mazoezi ya viungo yaani aerobics katika Viwanja vya Chuo Kikuu Ardhi. Mazoezi hayo yametanguliwa na matembezi ya umbali wa Kilometa tatu (3km) kuanzia jengo la Utawala la Chuo Kikuu Ardhi kuzunguka maeneo ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam na badae kurudi katika viwanja vya Chuo Kikuu Ardhi na kuendelea na mazoezi mengine ya viungo (aerobics).
Mazoezi hayo yamehudhuliwa na watumishi mbalimbali wa Chuo Kikuu Ardhi wakiongozwa na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango na Fedha na Mshauri wa Wanafunzi huku wanafunzi wakiongozwa na Raisi wa Serikali ya Wanafunzi, Makamu wa Raisi, Katibu Mkuu, Waziri wa Habari na Naibu Waziri Michezo.
Aidha baada ya mazoezi hayo Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma amewapongeza watumishi wote walio hudhuria mazoezi hayo huku akitoa rai kwa Watumishi wote na Wanafunzi kwa ujumla kuhudhuria kwa wingi kwenye zoezi hili endelevu. Pia amevipongeza vikundi mbalimbali ambavyo kwa namna moja au nyingine vimewezesha kufanyika kwa zoezi hilo. Vikundi hivyo ni pamoja na kikundi cha ARISA chini ya kiongozi wao Dr. Sarukele na kikundi cha Serikali ya Wanafunzi ARUSO chini ya Raisi wao Mh. Kiwango Erasmus,B.
Mazoezi ni afya karibuni tena tar 13/05/2017.
Endelea kutembelea ARUSO BLOG kupata Taarifa mbalimbali
0 comments:
Post a Comment